HAKUNA mpaka wala muda maalum wa kufanya tendo la ndoa na mpenzi wako,hiyo haina shaka.
Lakini kitaalamu kuna muda mzuri wa kuweza kufanya mapenzi ambao kila mmoja ataridhika ikiwa hakuna tatizo la kiafya baina ya wapenzi wawili.
JE,NI MUDA GANI?
Kitaalamu muda wa asubuhi kuanzia saa kumi alfajiri mpaka saa kumi na mbili asubuhi ndio muda mzuri wa kuweza kufanya penzi la kuridhisha.
KWANINI IWE ASUBUHI?
Asubuhi mara nyingi kwa mwanaume ndio muda mzuri sana kwasababu muda huo sehemu za siri za mwanaume zinakuwa na nguvu zaidi wakati wa asubuhi kuliko muda mwingine wowote kwa sababu zifuatazo
1.AMETOKA USINGIZINI
Kitaalamu mtu anayetoka usingizini anakuwa na akilli mpya,ameondoa uchovu, ameondoa msongo wa mawazo na anakuwa na akili mpya.
Mambo ambayo yanaathiri ufanisi wa tendo la ndoa ni uchovu,mawazo, hisia mbaya,hasira na usingizi kitaalam unaondoa mambo hayo.
2.MZUNGUKO WA DAMU UNAKUWA WA KASI
Mara nyingi mtu anayefanya kazi katika mazingira ya baridi huwa hachoki sana kuliko anayefanya kazi wakati wa joto kutokana mzunguko wa damu ambao ndio unaufanya mwili uwe na nguvu unakuwa wa kasi muda wa asubuhi na ili uume uwe imara lazima kuwe na kiwango cha kutosha cha mzunguko wa damu unaofika hapo.
Post a Comment