KATIKA ulimwengu wa sasa kila mtu
analilia penzi la kweli na kila anapojaribu anajikuta ni watu wale wale ambao
pengine wanasimuliwa pengine ni walaghai au wenye kuumiza mioyo ya watu na
kuwaachia maumivu ya penzi.
Ili kumjua huyo uliyekuwa naye ni
mpenzi wa kweli kwanza angalia sifa hizi
1.KUFICHA
SIRI
Mpenzi wa kweli huwa siku zote
huficha siri za ndani ya nyumba hata mlale njaa bado akiulizwa na watu hatatoa
aibu hiyo hata kwa ndugu yake,hata uwe na kilema fulani bado ataendela
kukusitiri,kinyume cha hivyo huyo si mkweli.
2.KUKUHURUMIA
Mpenzi mwenye mapenzi ya kweli
atakuwa na huruma na wewe kwa kila jambo,ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya watu
wanaoingia katika uhusiano wanaangalia hali ya kipato cha mtu.
Ukionekana una nafuu basi huyo mpenzi
atakuonyesha kila aina ya mapenzi ili mradi ujue kuwa ni mkweli,lakini kipato
kikiisha utaanza kuzigundua tabia zake halisi.
Lakini mwenye mapenzi ya kweli
hata uwe milionea yeye kila siku kwako atakuwa
ni mwenye kuzilinda mali zako na mipango yake itakuwa ni malengo atahakikisha
anchunga matumizi.
3.KUKUSAMEHE
UNAPOMKOSEA
Mwanamke/mwanamme aliyekupenda
kwa dhati siku zote huwa ni msamehevu kwako hata kosa liweje yeye ataumia
moyoni ila mwisho wa siku mtakaa pamoja mtasameheana na mambo yataisha kama
hakuna udhaifu uliotokea baina yenu.
Asiyekuwa na mapenzi ya kweli
kwako unapomkosea atatumia hilo kosa kama fimbo ya kukudhalilisha mbele za watu
na siku zote atakuwa ni mwenye kuhesabu makosa.
4.KUONESHA
USHIRIKIANO KWENYE MAENDELEO NA NDUGU
Mpenzi mwenye mapenzi ya
kweli si mbinafsi siku zote atakuwa
mstari wa mbele katika maendeleo yenu,atakuwa mchumi,muadilifu na muwazi katika
mapato na matumizi.Asiyekuwa mkweli atakuwa ni mbadhirifu wa pesa na mali yeye
atajiangalia yeye tu.Pia hata kwa upeande wa ndugu zako lilitokea jambo atakuwa
kipaumbele.
Hata awe amekukuta na watoto
atawalea kama watoto wake.
1 comments:
Naitwa Noah kutoka Kenya mtaa wa bungoma,Niko na rafiki wa kike ambaye huwa natamani SANA niwe katika mahusiano na yeye lakini Kula nijaripupo kumuelezea hisia zangu kwake huwa anasema eti Mimi hua naongea vibaya,nashindwa kumuelewa.nifanyeje Mimi na roho yangu ishampenda
ReplyPost a Comment