MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi(CCM)katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 John Pombe Magufuli ni kama
ametengwa au amejitenga na chama chake kutokana na wachambuzi wa siasa katika
mambo yafuatayo.
Dalili za za wazi kwamba huenda
ametengwa au maejitenga na chama chake
ni hiz zifuatazo.
1.MABADILIKO
Magufuli inasemekana hafuati sera
za chama chake isipokuwa anabuni sera zake au kuiga sera za Lowasa wa UKAWA kwa
hilo neno MABADILIKO.
Kwa mujibu wa aziri Mkuu mstaafu
Fedrick Sumaye amesema kuwa Magufuli hawezi kuleta mabadiliko ndani ya CCM
kutokana CCM imetawaliwa na rushwa,pia wizara yake ya Ujenzi inakabiliwa na ufisadi mkubwa na matumizi
mabaya ya fedha.
2.
NITAWASHUGHULIKIA MAFISADI.
Moja katika kampeni zake ni
kuwashughulikia mafisadi, je atawezaje kuwashughulikia mafisadi wakati yeye yupo
ndani ya CCM ambapo ndio kunalalamikiwa kuna mafisadi wakubwa?
3.CHAMA NA
MAGUFULI.
Siku zote katika mabango ya
kampeni za CCM huandikwa kwa mfano
CHAGUA FULANI,CHAGUA CCM lakini safari hii mabango yake mengi yameandikwa
CHAGUA MAGUFULI Hapa Kazi Tu, Hakuna CHAGUA MAGUFULI,CHAGUA CCM.
4.KAMPENI NA
WASTAAFU.
Siku zote viongozi wakuu wa CCM
katika maeneo ya upinzani huwa wanaongeza nguvu kwa viongozi wakuu wastaafu wa
nchi kama vile marais na mawaziri wakuu wastaafu lakini safari hii Magufuli anakwenda peke yake
ndiyo maana anaongea sera ambazo haziendani na Chama chake.
Post a Comment