MAMBO vipi
wapendwa? Je,uliwahi kukutana na kauli
hii “Wanawake wanene ni wavivu katika mapenzi kuliko wanawake wembamba”.
Kama uliwahi
kukutana nayo je,ulishakutana na aina zote mbili za wanawake katika maisha yako
ya mapenzi? Kama ndiyo je,unaikubali hiyo kauli?
Wapendwa
ukweli ni kwamba mchezo wa mapenzi hauna
aina ya umbo kuwa ndiyo bora zaidi kuliko umbo fulani si kweli.
Mapenzi ni
sanaa ambayo haihitaji uvivu katika uwajibikaji huo ndiyo usahihi wa mambo
kama mwanamke akiwa mvivu basi utamuona
hajui mapenzi.
Kuna wanawake
wengine ni wanene wa maumbo yao lakini
wanajua kulitendea haki tendo la ndoa kuliko wanawake wembamba na ukashangaa,kinachotakiwa
hapo ni ubunifu wa mitindo mbalimbali kitandani.
Na kuna
wanawake wengine ni wembamba lakini wakiwa katika suala zima la mapenzi wanakuwa ni wavivu na hawajui kulitendea haki tendo mpaka ukamchukia.
Kiuhalisia
USIHUKUMU KUTOKANA NA UMBO,MAPENZI NI UWAJIBIKAJI kama mpenzi wako hajitumi
ipasavyo kaeni chini muongee mjue wapi pa kurekebisha ili kila mmoja aridhike na mwenzake kuliko kutoleana
siri zenu nje.
Fahamu kwamba
mwenyezi mungu ni mjuzi katika uumbaji wake, wewe ukimuona hafai wengine
wanavutiwa naye ,usimseme vibaya ukampotezea kheri zake kwa wengine kwani dunia
hii si lazima watu wote wawe sawa unavyotaka wewe.
Post a Comment