JEZI feki za timu ya Simba zimeanza kuuzwa katika
maeneo mbalimbali kuzunguka uwanja wa Mkwakwani jijini hapa ikiwa ni maandalizi
ya ufunguzi wa pazia la ligi kuu ambapo timu ya Simba itakuwa wenyeji wa
African Sports “Wana kimanumanu” kesho (jumamosi) katika uwanja huo.
Mwangaza blog imeshuhudia wafanyabiashara ndogo ndogo
“machinga” wakizisambaza chini jezi hizo
ambazo ni feki kutokana materials yake,pamoja na rangi yake kupauka,pia hazina
nembo ya timu hiyo zikitundikwa kwenye miti iliyopo nje ya uwanja huo.
Aidha mbali na
jezi hizo kupangwa uwanjani hapo pia wafanyabiashara wengine wadogowadogo wanazitembeza mitaani jezi hizo.
Aidha jezi hizo
zinauzwa kwa bei tofauti kutokana na aina ya jezi unayoichagua na inauzwa kwa
kiwango cha chini kuanzia elfu tano.
Post a Comment