UKARABATI wa uwanja wa Mkwakwani jijini hapa umekamilika
kwa asilimia tisini na upo tayari kwa ligi kuu.
Leo jumatano Mwangaza blog imetembelea uwanjani
hapo na kushuhudia mafundi wa kuchomelea wakiwa katika hatua za mwisho za
kuchomelea uzio unaotenganisha eneo la kuchezea na jukwaa la mashabiki
kuzunguka uwanja.
Kwa upande wa
vyoo vya wachezaji na vyumba vya kubadilishia wachezaji navyo vimekarabatiwa
vizuri ambapo vyoo vimewekwa vigae vya sakafu(tiles) vipya na kuta kupakwa
rangi ambapo upande wa kuchezea (pitch) nao nyasi zimeota vizuri ambapo zoezi
la kumwagilia maji linafanyika vizuri ili kuzistawisha nyasi hizo.
Akizungumza na blog hii baada ya kutembelea uwanja huo mjumbe wa TFF mkoa wa Tanga
Halidi Abdallah amesema kuwa Simba wakiwasili muda wowote wana ruksa ya
kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi.
Post a Comment