MGOMBEA mwenza wa urais wa UKAWA (CHADEMA)Juma
Duni Haji amesema kuwa rasilimali zilizopo nchini zingetumika ipasavyo
zingeondoa matatizo ya umaskini yanayowakumba watanzania.
Duni ameyasema
hayo katika mkutano wake wa kampeni
uliofanyika(leo)jumapili Septemba
6,2015 katika uwanja wa ng’ombe maarufu (CHADEMA Square) Muheza mjini wilayani
humo mkoani Tanga.
Amesema kuwa
ubinafsi wa viongozi na sera mbaya za Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika kuzitumia
rasilimali zilizopo nchini ndiyo mambo yaliyosababisha watanzania wengi kuwa katika tabaka la chini la maisha.
“Tanzania tuna
mbuga za wanyama,madini,gesi asilia,bahari lakini hazitumiki ipasavyo kutokana
na uroho wa viongozi pamoja na sera mbovu za CCM,laiti kama zinawafaidisha
watanzania ipasavyo,hakuna mtanzania angeishi maisha ya umaskini”alisema.
Aidha
amewaomba watanzania wapuuze sera na maneno
ya kuwagawanya kutokana na umoja wao wa vyama,bali waendelee kuungana mpaka siku ya uchaguzi ili walete mabadiliko
ya uongozi.
“Kuna watu ni
mamluki wanatumiwa kutugawanya kwa
kutokukubali baadhi ya wagombea katika UKAWA ili msipige kura,nawaambie mkichagua
mgombea yeyote kati yao katika vyama vinavyounda UKAWA mtakuwa mpeipigia UKAWA”alisema.
Juma Duni Haji
yupo katika ziara ya kampeni mkoani hapa katika kutangaza sera za UKAWA na
kuhamasisha wananchi katika kupiga kura ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Post a Comment