TANGA
IKIWA imebaki wiki moja kwa ligi kuu ya Vodacom nchini,timu mahasimu za mkoani Tanga African Sports na Coastal Union leo (jumamosi) 05/09/2015 zinashuka dimbani katika uwanja wa Mkwakwani jijini humo katika mechi ya kirafiki itakayofanyika majira ya saa kumi jioni.
Timu hizo kongwe mkoani hapa zimeleta ladha ya pekee baada ya African Sports"Wana kimanumanu" kurejea ligi kuu baada ya kupotea kwa takribani miaka ishirini katika ramani ya soka nchini.
Baada ya mechi hii ya leo(jumamosi)African Sports itakuwa ni kipimo chake cha mwisho kabla ya kuwakaribisha Wana msimbazi (Simba Sports Club) katika ufunguzi wa pazia la ligi kuu wiki ijayo Septemba 12,2015 katika uwanja huo wa Mkwakwani.
Coastal Union kwa upande wake ambayo msimu huu imesajili chipukizi wengi katika kikosi chake, nao huu utakuwa mtihani wao wa mwisho kabla ya kuwafuata timu ya Yanga katika uwanja wa taifa Septemba 13,2015
Post a Comment