DUNIA nzima inashuhudia Tanzania mwaka huu(2015) ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa tano tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa nchini Tanzania.
Kila kipindi Demokrasia imekuwa ikikuwa kwa kasi sana kwa kuanzishwa vyama vya kisiasa,kati ya vyama hivyo vingine vimedumu mpaka leo tangu kuanzishwa kwake,vingine vimepotea na vingine vipya vikianzishwa kila karibia na kipindi cha uchaguzi mkuu.
Katika kila kipindi chama cha upinzani chenye nguvu kwa wakati huo kimekuwa na idadi kubwa ya mashabiki na wanasiasa lakini katika uchaguzi unapofika unasikia kimepata kura kidogo tofauti na ilivyofikiriwa.
Mwaka 1995 NCCR-Mageuzi chini ya Augustino Mrema kilikuwa na nguvu, 2000 CUF chini Profesa Ibrahim Lipumba(Tanzania Bara) na Maalim Seif Sharif Hamadi(Zanzibar), 2005 Freeman Mbowe na 2010 -CHADEMA chini ya mgombea urais Dkt.Wilbrod Slaa lakini mwishowe CCM ilibaki madarakani.
Mwaka huu tumeona vyama hivyo (CUF,CHADEMA,NLD na NCCR-MAGEUZI) vimeungana na kutengeneza umoja wao (UKAWA) ambao asili yake ulianzia katika bunge maalum la Katiba baada ya kutoridhishwa na kupingwa Rasimu ya Katiba mpya ya maoni ya Wananchi chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Sinde Warioba kupingwa waziwazi na wabunge wa CCM.
Umoja huo(UKAWA) unamsimamisha Edward N.Lowassa wakati CCM ikimsimamisha John Pombe Magufuli.
Kila ukitizama na kufuatilia mikutano ya kampeni ya wanasiasa hao unakuta imejaza watu. Swali la kujiuliza Je,wingi huo wa watu ndio ushindi wa chama au ni kukua kwa Demokrasia nchini?
Post a Comment