Mkapa: CCM ndio chama cha ukombozi Tanzania,Africa





RAIS mstaafu wa awamu ya tatu nchini Benjamin Mkapa amesema kuwa chama cha  mapinduzi ndio chama pekee cha ukombozi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Mkapa ameyasema hayo leo  17/10/2015 jumamosi  katika uwanja wa jitegemee wilayani Muheza mkoani  Tanga majira ya saa kumi jioni wakati akimnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM John  Pombe Magufuli na mgombea ubunge jimbo la Muheza balozi Adadi Rajabu.

Amesema kuwa  watu wanaosema CCM haikufanya kitu katika miaka yake ya utawala Tanzania hawajui historia ya nchi hii.

Amesema kuwa  chama hicho pia kimefanya mapambano ya ukombozi wa baadhi ya nchi za Afrika kama Zimbabwe,Msumbiji na Afrika ya Kusini na kinaheshimika kitaifa na kimataifa.

“Watu wanaosema kuwa CCM haikufanya  chochote katika uwtawala wake wao  hawajui historia ya nchi, chama hiki kinaheshimika kitaifa na kimataifa” alisema.

Aidha amesema kuwa chama hicho hakikutenda haki katika harakati za kuchagua mgombea urais ndani ya chama hicho si kweli.

Badala yake amesema kuwa chama hicho kimetumia taratibu zile zile za kutafuta  mgombea wa urais kwa kuangalia taarifa zake binafsi,uadilifu, na zimepitiwa taratibu zote za kamati ya maadili,baraza la wazee,halmashauri kuu ya taifa na mkutano mkuu.
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.

Post a Comment

CodeNirvana
Older Posts
© Copyright Mwangaza Blog Published.. Blogger Templates
Back To Top