RAIS mstaafu wa awamu ya tatu nchini Benjamin
Mkapa amesema kuwa chama cha mapinduzi
ndio chama pekee cha ukombozi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Mkapa
ameyasema hayo leo 17/10/2015
jumamosi katika uwanja wa jitegemee wilayani
Muheza mkoani Tanga majira ya saa kumi jioni
wakati akimnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Pombe Magufuli na mgombea ubunge jimbo la
Muheza balozi Adadi Rajabu.
Amesema
kuwa watu wanaosema CCM haikufanya kitu
katika miaka yake ya utawala Tanzania hawajui historia ya nchi hii.
Amesema
kuwa chama hicho pia kimefanya mapambano
ya ukombozi wa baadhi ya nchi za Afrika kama Zimbabwe,Msumbiji na Afrika ya
Kusini na kinaheshimika kitaifa na kimataifa.
“Watu
wanaosema kuwa CCM haikufanya chochote
katika uwtawala wake wao hawajui
historia ya nchi, chama hiki kinaheshimika kitaifa na kimataifa” alisema.
Aidha amesema
kuwa chama hicho hakikutenda haki katika harakati za kuchagua mgombea urais
ndani ya chama hicho si kweli.
Badala yake amesema
kuwa chama hicho kimetumia taratibu zile zile za kutafuta mgombea wa urais kwa kuangalia taarifa zake
binafsi,uadilifu, na zimepitiwa taratibu zote za kamati ya maadili,baraza la
wazee,halmashauri kuu ya taifa na mkutano mkuu.