KUMBUKA KATIKA UZINDUZI WA SAFARI YA MATUMAINI WAKATI EDWARD LOWASSA AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS NDANI YA CCM KATIKA UWANJA WA SHEKHE AMRI ABEID PALE ARUSHA YEYE NDIYE ALIKUWA MZEE PEKEE WA CCM ALIYEHUDHURIA SHEREHE HIZO.
NENO LAKE KUU NI :KATIBA YA CCM ILIKIUKWA KATIKA MCHAKATO WA WAGOMBEA URAIS NDANI YA CCM.
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru.
Kingunge amezungumza leo mbele ya waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es salaam.
Kingune amesema hawezi kuhimili chama kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi wake utawasumbua baadhi ya ndugu zake, wazee na makada wengine.
Mwanasiasa huyo amesema kwa sasa hakusudii kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.
Pia amesema yeye ni raia na ana haki zake za kisiasa na kijamii na ataendelea kuwa na mahusiano mazuri na nchi yake..”Hali ya sasa jinsi ninavyoona vijana, wafanyakazi, wakulima wanataka mabadiliko na mimi nipo upande wa mabadiliko kwa sababu wakati tukiwa TANU tulifanya mabadiliko na kuunda CCM”…KINGUNGE
Post a Comment