BAADHI ya wana CCM waliokuja kumpokea mgombea mwenza wa urais kupitia CCM leo tarehe 21/09/2015 katika uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza wamekiona cha moto baada ya kushindishwa na njaa kuanzia saa tano asubuhi mapa saa kumi na nusu alipowasili mgombea huyo akitokea wilaya ya Pangani.
Wana CCM hao ambao wameletwa kutoka vijijini vya wilaya ya Muheza wakitumia usafiri wa magairi kumi na nane aina ya fuso,Canter na Ciosater na Hiace walijikuta wakishinda na njaa bila kutarajia baada ya kuambiwa mombea angewasili kmajira ya saa sita mchana uwanjani hapo.
Wana CCM hao ambao wengi walikuwa wanawake na wazee walisikika wakilalamika kushinda na njaa bila ya hata ya kupewa pesa ya maji ya kunnywa kwa kuambia wakipewa itaonekana wanahongwa hivyo wavumilie mpaka wakirudi makwao.
WanaCCM hao wakiwa katika hali ya kukata tamaa huku wengine wakija na watoto wadogo na wazee hawakuweza kuvumila njaa wakaanza kulalamika ndio wasamaria wema wakawanunulia chakula wengine wakala kwa ndugu zao wanaoishi hapa mjini.
Snura ndiye aliyewarudisha wasanii hao baada ya kuimba wimbo wake wa "majanga" mpaka mgombea mwenza alipowasili ambapo kitu cha kwanza aliwaomba radhi.
Post a Comment