MGOMBEA mweza wa urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ikiwa serikali ijayo ya CCM itakapoingia madarakani itakamilisha mambo ambayo yaliachwa na serikali za awamu zilizopita.
Ameyasema hayo wakati akiwahutubia wana CCM wa Muheza katika uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga.
1.Barabara
Amesema kuwa kwa upande wa Muheza kama wakipewa ridhaa ya kuongoza nchi wataijenga Barabara ya Muheza-Amani yenye urefu wa kilometa 42 katika kiwango cha lami.
2.Elimu
Kwa upande wa elimu amesema kuwa elimu itakuwa bure kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha nne,isipokuwa amesema kuwa uendeshaji wa shule utakuwa chini ya serikali isipokuwa michango ya maendeleo ya shule itakuwa chini ya kamati za shule.
3.Maji
Kwa upande wa Maji wakazi wa Muheza wameahidiwa kuletewa maji kutoka mto Zigi mpaka Muheza mjini ifikapo mwakani ila akasema kuwa maendeleo ni safari kuna yatakayowafikia mwanzo,wengine katikati na wengine mwisho.
4.Afya
Kwa upande wa afya amesema serikali yake itaajenga hospitali za wilaya pamoja na kuongeza wataalamu na vifaa tiba nchi nzima.
5.Ardhi
Kuhusu ardhi amesema kuwa serikali itagawa ardhi ambayo haitumiki kwa wananchi na mashamba makubwa ya mkonge ambayo hayafanyi kazi hati zake zipo mezani kwa rais zinasubiri kubadilishwa matumizi.
Post a Comment