WAKATI
mwingine mpango wa mungu unapotaka kutimia unakuwa na sababu!,hata adui au
ugomvi baina ya wawili au pande mbili unaweza
kuwa ndiyo sababu ya mpango wa mungu kutimia au kutimia maslahi fulani.
Je,unajuwa
kuwa UKAWA imesababishwa na wana CCM wenyewe? Ndiyo,amini hivyo sababu kubwa ya
kuundwa kwa UKAWA ni rasimu ya Katiba mpya ya Jaji Joseph Sinde Warioba
kupingwa na wabunge wa CCM.
1.Sababu kubwa
ya kwanza ni wabunge wa CCM kupinga serikali tatu ambayo ni maoni ya wananchi
na kutaka serikali mbili za muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
2.Walikataa
tunu za uwazi na uwajibikaji kwa sababu ya ufisadi katika halmashauri na kutoa
ahadi bila ya kuzitekeleza.
Baada ya hapo
wabunge wa upinzani kupitia vyama vya
NLD,CUF,CHADEMA na NCCR-Mageuzi wakasusia bunge hilo maalum na kuunda Umoja wa
Katiba ya Wananchi(UKAWA) wakawa wanawaelimisha wananchi kuhusu kuipinga rasimu
hiyo ya katiba nje ya bunge.
Mwenyekiti wa bunge
hilo maalum la katiba alikuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Samuel
Sitta ambaye pia alikuwa Spika wa bunge mwaka 2005-2010.
Alama nyingine
ya UKAWA kutokana na CCM hata mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA Edward Lowassa
alijiunga na CHADEMA baada ya jina lake
kukatwa katika kura za maoni za wagombea urais ndani ya CCM ambapo jina lake
hata tano bora halikuingizwa licha ya kuwa na mvuto mkubwa ndani na nje ya
chama.
Post a Comment